Baada ya Alikiba kufunga ndoa Jokate akapata mpenzi mpya

Baada ya msanii Alikiba kuoa, maneno mengi na maswali yamekuwa yakielekezwa kwa mrembo Jokate Mwegelo.


Sababu ni kwamba mara kadhaa mrembo huyo alidaiwa kuwa katika mahusiano na Alikiba, hivyo kitendo cha Alikiba kuoa mwanamke mwingine kilizidi kuibua mijadala ya hapa na pale kuhusu Jokate.

Sasa muimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amemuelezaJokate kuwa asijali kwa kuwa ndoa inakuja, hata hivyo haijafahamika iwapo ni yao wawili au laa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Usihofu Mungu hajakuacha Jokate Mwegelo yakwetu inakuja, tv zote zitakuwa live ukumbini hadi wasafi tv,” amesema Mbasha.

Katika kuhadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa March 20, 2018 Jokate aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa ingawa hakuweka wazi ni nani atahusika katika ndoa hiyo.

Utakumbuka pia muimbaji Mbasha kwa sasa hayupo katika ndoa na hii ni baada ya kuachana na aliyekuwa baby mama wake, Madam Flora ambaye aliolewa April 30, 2017 na Daudi Kusekwa.

Shabani Chris

JIUNGE NA CELEBZMAGAZINE.COM SASA
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *