Wenger kuondoka na kitita kinono cha fedha

Klabu ya Arsenal inatarajia kuukatisha mkataba wa meneja wake, Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu na kumlipa kitita cha pauni milioni 11.

Wenger ambaye ni raia wa Ufaransa hapo jana alitangaza kuondoka Emirates baada ya ufalme wake wa miaka 22 kwisha tangu alivyoanza kuiyongoza klabu hiyo mwaka 1996.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 amesikika akisema kuwa ni muda muafaka kwake sasa kung’atuka huku taarifa za chini zikidaiwa kuwa nikutokana na shinikizo la mmiliki wa timu hiyo, Stan Kroenke aliyemtaka kufanya hivyo.

Reports claim that Wenger lost the support of owner Stan Kroenke, who decided to act

Wenger akisalimiana na mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke

Kwamujibu wa chombo cha The Sun inaelezwa kuwa, Wenger amepoteza ushirikiano kutoka kwa mmiliki wa timu hiyo, Stan Kroenke.

Mmiliki huyo inadaiwa kuwa alikuwa akimtupia lawama Wenger kuwa hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu na hivyo kulazimisha kulipwa fedha zake zote za mwaka wake mmoja wa mwisho.

 

Shabani Chris

JIUNGE NA CELEBZMAGAZINE.COM SASA




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *